Na Wilbert Molandi Dar es Salaam
STRAIKA wa kutumainiwa wa El Merreikh ya Sudan, Allan Wanga, raia wa Kenya, ameonyesha nia ya kutua Msimbazi ikiwa Simba itatimiza matakwa yake.Straika huyo, alitakiwa kutua Azam FC kwenye usajili mkubwa wa Ligi Kuu Bara mwanzoni mwa msimu huu, lakini ikashindikana kutokana na kubanwa na mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakiza El Merreikh.
Mkenya huyo anayesifika kwa kuzifumania nyavu, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayomhitaji kutokana na kubakiza mwezi mmoja.Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, hivi karibuni alitamka kuwa katika usajili wake wa msimu ujao, lazima wamsajili mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya Simba, mmoja wa viongozi wa timu hiyo amekabidhiwa jukumu la kuhakikisha anafanikisha usajili wa mshambuliaji huyo.Chanzo hicho kilisema, mazungumzo kati ya Wanga na Simba yapo katika hatua nzuri.
Kiliongeza kuwa, mshambuliaji huyo aliyeitoa Azam FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa bao kali la kichwa, mwenyewe anaonekana kuridhishwa kutua Simba kutokana na mazungumzo yanayoendelea.
“Kocha anahitaji mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao akiwa ndani au nje ya 18, kutoka ndani au nje ya nchi.
“Na wapo kwenye mazungumzo awali na Wanga ili atue kuichezea Simba kwenye msimu ujao wa ligi kuu, tunaamini ni mshambuliaji mwenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kufunga mabao,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wanga kuhusiana na taarifa hizo, alisema: “Mimi ni mchezaji huru hivi sasa kutokana na mkataba wangu kumalizika mwezi ujao. Simba waje.
“Ninaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayonihitaji, zipo baadhi za timu kutoka huko Tanzania na Afrika Kusini nilizoanza nazo mazungumzo ya awali.
“Afrika Kusini timu inayonihitaji ni Bidvest Wits inayoshiriki ligi kuu, lakini binafsi sipendi kwenda huko kwa sababu ni mbali na nyumbani, mimi ninataka kuzichezea timu zilizopo karibu na nyumbani,” alisema Wanga.
Hivi karibuni, Championi lilizungumza na Rais wa Simba, Evans Aveva, ambaye alisema kwa mujibu wa ripoti ya kocha, wanahitaji straika mmoja mwenye uchu wa mabao. “Kocha anataka mshambuliaji mmoja, kwa hiyo kazi yetu kubwa wakati wa usajili itakuwa ni kusaka mshambuliaji,” alisema Aveva.
Simba inaonekana kupunguza makali kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kumuachia Amissi Tambwe aende Yanga na sasa inamtegemea zaidi Emmanuel Okwi ambaye msimu huu amefunga mabao saba kwenye ligi. Elias Maguli aliyesajiliwa akitokea Ruvu Shooting ameonekana kushindwa kuvaa viatu vya Tambwe. Mpaka sasa ana mabao matatu tu kwenye ligi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.