Monday, April 27, 2015

Anonymous

INATISHA SANA! Siku 4 tu baada ya harusi, Mume amfanyia ukatili huu wa kutisha mkewe!

Handcuffed Prisoner
Wivu wa mapenzi upo, lakini huyu jamaa aliamua kufanya ukatili kwa mpenzi wake, ilikuwa siku nne tu baada ya kufunga ndoa zao.

Hii stori imetoka Brazil baada ya mume kuamua kumuua mke wake kisa tu huangaliwa na wanaume ikiwa ni siku ya nne tu tangu afunge naye ndoa kanisani.

Wawili hao ambao walikuwa wakiishi katika mji wa Rio De Janeiro, kwa sasa mwanaume huyo ameshikiliwa na polisi na kufunguliwa kesi ya mauaji.

Mwanaume huyo Vieira Severiano alimuua mkewe Cixera Alves De Sena ambaye alikuwa ni mcheza shoo katika bustani ya sehemu waliyokuwa wakiishi ambapo camera ziliweza kunasa tukio zima.

Video hiyo ilimwonyesha mwanaume huyo akigombana na mkewe kwa muda kabla ya kumpiga risasi tano usoni iliyosababisha kupoteza maisha yake.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.