Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

HUKUMU YA MORSI LEO


Mohammed Morsi.
MAHAKAMA nchini Misri inatarajia kutoa hukumu kwenye kesi kadhaa zinazomkabili rais wa zamani, Mohammed Morsi ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013.
Mosri anakabiliwa na kesi pamoja na viongozi wengine wa Kundi la Muslim Brotherhood kwa kuwachochea wafuasi kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwaka 2012. 

Mawakili wanaomtetea Mosri wanasema kuwa huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo. Mamia ya wafuasi wa Kundi la Muslim Brotherhood wamehukumiwa kifo katika mikakati ya kukabiliana na kundi hilo lililopigwa marufuku na rais wa sasa Abdul Fattah al-Sisi.
Kundi la Muslim Brotherhood limemlaumu rais kwa kutumia mahakama kama silaha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.