WAKATI taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao 
ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat 
Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la 
kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake. 
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo 
maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo
 walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa 
imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya 
waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita. 
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na 
viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri 
kiongozi huyo afikie kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano 
zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu 
ambapo taarifa za kina kuhusu kilichojiri huko zikiwa bado 
hazijapatikana.
(Habari/Picha:Chande Abdallah, Makongoro Oging, Deogratius Mongela na Issa Mnally)

Note: Only a member of this blog may post a comment.