Jamaa huyu amefungwa kwenye gereza la Naivasha Kenya, kilichoipa uzito zaidi story hii ni ishu ya kuwepo kwa wafungwa wachache wazungu katika magereza mengi.
Mfungwa huyo anaitwa Joachim alifungwa
mwaka 2007 baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kukutwa na dawa za
kulevya, gerezani ana jukumu jingine ambalo limemuweka kwenye nafasi
tofauti na wafungwa wengine.
Jamaa ni engineer wa umeme, gerezani ni
fundi wa kutegemewa kwa hiyo ikitokea kama tatizo la kiufundi kwenye
masuala ya umeme na vifaa vingine kama TV basi yupo kwa ajili
ya kurekebisha kila kitu.
Joachim
anasifiwa kuwa na mwenendo mzuri, kapewa sare tofauti na wafungwa
wengine pia, unaweza kumcheki kwenye hii video hapa maisha yake ya
gerezani kwa ufupi..


Note: Only a member of this blog may post a comment.