Tuesday, March 10, 2015

Anonymous

LOVE YA UKWELI: Shabiki wa Rihanna kaamua kujioneshea upendo wa nguvu kwa style hii



riri23
Mapenzi ya mashabiki kwa mastaa mbalimbali huwa yanaonekana kwa njia nyingi, wengine wanavaa kama mastaa hao, wengine wananyoa, au kusuka.. Yani shabibiki anafanya chochote ili kuonyesha jinsi ambavyo ana mapenzi na staa huyo.
saraa
Huyu ni shabiki wa nguvu wa Rihanna, ameamua kujichora tattoo 14 mwilini mwake kutokana na mapenzi aliyonayo kwa mwanamuziki huyo.

Sara Ridge ni shabiki huyo raia wa Afrika Kusini, ana tattoo saba zenye sura ya Rihanna katika mwili wake na ametumia zaidi ya paundi 2,000 kama gharama ya kujichora, katumia saa zaidi ya 48 mpaka zoezi lote limekamilika.

Mbali na picha hizo sehemu nyingine amechora maandishi ya mashairi ya nyimbo za staa huyo.
riri24
rrrr
Mama yake Sarah alimkataza mwanae kuchora tattoo hizo akimsihi kwamba huenda siku moja akajutia kufanya hivyo.
ririi22
“Marafiki zangu na ndugu zangu hawakukubaliana na maamuzi yangu lakini kwa kuwa mwenyewe nilitaka kufanya hivyo, sikupenda kusikiliza ushauri wa mtu yoyote… siwezi kuja kujutia“– Sara.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.