Tuesday, March 10, 2015

Anonymous

VIDEO [BALAA TUPU] Vurugu zilizotokea Bungeni leo unaweza kutazama hapa !

Leo ukumbi wa baraza la Kaunti ya Nakuru Kenya umegeuka  kuwa uwanja wa ngumi baada ya Wabunge kupigana kutokana na kuwepo kwa mvutano kati ya Wabunge wanaomuunga mkono Spika Susan Kihika aliyefukuzwa hivi karibuni na Wabunge wengine kumtaka Naibu Spika Samuel Tunui aendeleze vikao vya Bunge leo, huku Naibu Spika huyo akidai kushambuliwa na wahuni waliokodishwa na Spika.

Kulikuwa na muswada uliokuwa upendekeze kanuni kuhusu jinsi ya kumuondoa Naibu  Spika, Samuel Tunui na wenyeviti wa kamati mbAalimbali wanaodaiwa kupinga uongozi wa Spika ambao Wabunge hao bado hawajakubaliana kuupitisha muswada huo.

Taarifa hiyo iliyoripotiwa na TV ya K24 bonyeza play hapakuitazama…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.