Sunday, March 29, 2015

Anonymous

URAIS 2015: Lowassa Aongoza, Mwingulu Nchemba Ang'ara Kama Kijana Anayekubalika Zaidi

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Positive Thinkers Tanzania imetoa ripoti yake ya utafiti kuhusu mwanasiasa anayekubalika zaidi na wananchi katika nafasi ya Rais ajaye.

Lowassa aongoza na nafasi ya 2 imeenda kwa Dr. Wilbroad Slaa huku Mwigulu Nchemba aking'ara kama kijana aliyeongoza kwa kukubalika kwa kukamata namba 3.

Ifuatayo ni orodha ya wanasiasa waliongia 10 bora na asilimia ya kura walizopata.
1. Edward Lowassa 22.8%
2. Wilbroad Slaa 19.5%
3. Mwigulu Nchemba 10.6%
4. Ibrahim Lipumba 8.9%
5. John Magufuli 6.8
6. Zitto Kabwe 6.7 %
7. Bernard Membe 5.9%
8. Mizengo Pinda 3.2%
9. January Makamba 1.6%
10. Mark Mwandosya 1.2
Kwa upande wako wewe, yupi unampa kura yako hapo?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.