Monday, March 16, 2015

Anonymous

[PICHAZ+MAELEZO] Viwanja 10 vinavyoongoza kwa kuchukua idadi kubwa ya mashabiki duniani


Mchezo wa soka umeendelea kuwa mchezo unaoongoza kwa kupendwa na watu wengi zaidi duniani na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki pengine kuliko mchezo mwingine wowote.

Tumeshuhudia kwa timu zilizoendelea wanaweka nguvu kubwa kuwekeza sio kwenye wachezaji wakali uwanjani bali hata kuwa na viwanja vizuri.

Leo nakuwekea hii ya list ambayo Hivi ni viwanja 10 ambavyo vinaongoza kwa kuchukua idadi kubwa ya mashabiki duniani:-
1. Rungrado May Day Stadium

Upo Korea Kaskazini: Una uwezo wa kuchukua mashabiki 150,000

2. Salt Lake Stadium

Upo India: una uwezo wa kuchukua mashabiki 131,000

3. Bukit Jalil National Stadium

Upo Kuala Lumpur Malaysia, una uwezo wa kuchukua jumla ya mashabiki 100,411

4. Camp Nou

Upo Hispania, una uwezo wa kuchukua mashabiki 99,786. Huu ni Uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Barcelona.

5. FNB Stadium

Upo Johannesburg Afrika Kusini, una uwezo wa kuchukua mashabiki 94,736. Jina maarufu ambalo Uwanja huu unaitwa ni Soccer City.

6. Rose Bowl Stadium

Upo USA, una uwezo wa kuchukua mashabiki 92,542 kwa wakati mmoja.

7. Cotton Bowl Stadium

Upo Dallas, Texas Marekani. una uwezo wa kuchukua mashabiki 92,100.

8. Memorial Stadium

Upo USA. Una uwezo wa kuchukua mashabiki 91,471

9. Wembley Stadium

Upo London, Uingereza: una uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000

10. Eden Garden

Upo Kolkata India: una uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.