Mwezi
uliopita tulisikia habari ya bibi harusi mmoja huko India kuolewa na
mgeni ambaye alikuwa amealikwa tu kwenye harusi baada ya mwanaume ambaye
ilikuwa afunge naye ndoa kuanguka ghafla kwa ugonjwa wa kifafa, dakika
chache kabla ya ndoa kufungwa.
Kuna
taarifa nyingine ambayo imepewa headlines, hii inahusu harusi moja
kushindwa kufanyika India kisa ni kitendo cha bwana harusi kufeli swali
la hesabu ya kawaida kabisa aliloulizwa na bibi harusi.
Walioshuhudia harusi hiyo wamesema bwana harusi aliulizwa swali hili; kuwa ”15+6=?“
Sherehe ya harusi hiyo iliharibika baada
ya bi harusi kuanza kuongea kwa hasira baada ya kukasirishwa na kitendo
cha mumewe huyo mtarajiwa kutoa jibu la hesabu hiyo kwamba ni 17.
Bibi harusi aliondoka jukwaani akiwa amekasirika na kusema hawezi kuolewa na mtu ambaye hakwenda shule.
Ndugu wa bwana na bibi harusi walikubaliana kurudishiana zawadi zote walizotoa kwa ajili ya sherehe ya wapendwa hao.
Asilimia kubwa ya ndoa za India hupangwa
na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza siku
ya sherehe ya harusi yao.
Baba yake na bibi harusi, Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika kijiji cha Rasulabad alisema kuwa mwanawe alishangaa kuwa mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa na elimu.
-via millardayo
-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.