Friday, March 13, 2015

Anonymous

Matokeo ya Man United na Arsenal kuna taarifa ya kusikitisha toka Kenya..

Stori ya mashabiki kujiua eti kisa timu yake imefungwa ama ina matokeo mabaya kwenye ligi sio ngeni kuzisikia.. Wapo ambao wanashindana wanaweka nyumba au hela, timu yake ikishindwa ishu inakuwa story tofauti.

Taarifa kutoka Kaunti ya Kilifi pwani ya Kenya mtu moja amejitoa uhai kwa kujitosa ndani ya bahari hindi kutoka kwa Daraja la Kilifi baada ya kukasirishwa na matokeo ya Robo fainali kombe la FA baina ya mahasimu wakubwa Uingereza Arsenal na Man United iliyochezwa jumanne usiku.

Mtu ambaye alizungumza na jamaa ambaye amejiua amesema kabla ya mechi shabiki huyo alikuwa akijigamba jinsi Man U watakavyowaadhibu Arsenal, lakini hali ikawa tofauti.

Kitambulisho cha mtu ambaye alijiua kutokana na matokeo mabaya ya Man U. James Macharia Teresia.
Ishu iko mikononi mwaPolisi ambao wanendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.