Monday, March 16, 2015

Anonymous

Ishu ya mtoto aliyefanyiwa ukatili kwa kuunguzwa na kisu cha moto imesikika#Hekaheka

Tukio lililosikika leo kwenye Hekaheka ni ishu ya mtoto wa mpangaji aliyemuunguza mjukuu wa mwenye nyumba kwa bahati mbaya wakati akicheza na wenzake, baadae mzazi wa mtoto huyo alikuja na kupewa taarifa za tukio hilo na kisha kumfanyia ukatili mtoto huyo.

Akisimulia tukio hilo mtoto huyo amesema alikuwa akitoka nje akiwa amebeba sufuria ndipo mtoto huyo akatokea akiwa anakimbia na kugongana nae na kukuunguza kwa bahati mbaya kichwani, baadae akiwa uwanjani baba wa mtoto huyo alimuita na kwenda nae nyumbani na kuweka kisu jikoni na kumchoma nacho sehemu mbalimbali za mwili wake kama kulipiza kisasi. 

Majirani baada ya kugundua tukio hilo waliamua kwenda kushtaki Serikali za mitaa kutokana na mama huyo kuogopa kutoa taarifa akihofia kufukuzwa kwenye nyumba hiyo, Polisi walifika eneo hilo watu wao wakaanza kuwarushia maneno, kutokana na wingi wao wakaamua kuondoka na kwenda kuchukua gari ya Polisi kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.