Monday, March 16, 2015

Anonymous

HATIMAYE Zlatan Ibrahimovic "KADABRA" aomba msamaha!

Nyota huyo alijibu kwa hasira kuwa Ufaransa haiistahili PSG
Mshambuliaji wa Pari St-Germain Zlatan Ibrahimovic ameomba radhi baada ya kusema Ufarana haiistahili PSG.
Dongo la Ibrahimovic lilikuja baada ya kikosi chake kufungwa 3-2 kwenye Ligue 1 na Bordeaux siku ya Jumapili. 

Waziri wa michezo wa Ufaransa Patrick Kanner amemtaka Ibrahimovic kuomba msamaha na baadae kupendekeza ‘kukaribisha msamaha kutoka kwa bingwa hodari.” 

Nyota huyo alijibu kwa hasira kuwa Ufaransa haiistahili PSG
Mswidi, 33, alisema: “Nilikuwa nazungumza kwa sasa. Maneno yangu hayakumaanisha Ufaransa na watu wa Ufaransa.” 

Ibrahimovic, ambaye pia alimkosoa mwamuzi Lionel Jaffredo, aliongeza kuwa, “alikuwa anazungumzia soka ba sio kitu kingine” na aliomba msamaha ‘endapo watu walihisi kukosewa.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.