Monday, February 9, 2015

Anonymous

ZIMAMOTO YAZUNGUMZIA FAMILIA ILIYOTEKETEA KWA MOTO

Inspekta  Puyo  Nzalayaimis  akisoma tamko mbele ya waandishi wa habari (hawako pichani).
Nzalayaimisi  akisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari.
Wanahabari waliofika katika tukio hilo.
JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini limesema ukosefu wa taarifa kamili kuhusu eneo la ajali ya moto ambayo ilitokea Februari 7 mwaka huu na kuua watu sita wa familia moja katika Kata ya Kipawa, Mtaa wa Kipunguni ‘A’ jijini Dar ndiyo ulisababisha jeshi hilo kuchelewa kufika katika eneo hilo na kufanya uokoaji. 

Hayo yalisemwa na msemaji wa jeshi hilo, Inspekta Puyo Nzalayaimis  leo jijini kuhusiana  na nyumba ya David Mpira ambaye  naye alifariki katika tukio hilo ambapo nyumba yake ilianza kuungua usiku ambapo jeshi lake lilifika saa 12 alfajiri na kukuta nyumba yote imeteketea na moto kuwaua watu wote waliokuwa ndani. 

Ofisa huyo aliwataka wananchi kutoa taarifa mapema ya tukio husika  kwa kupiga namba ya dharura 114  ili kuliwezesha jeshi kufika kwa muda mwafaka,  na kwa mtu anayetoa taarifa kuhakikisha anatoa maelezo ya kina ya eneo la tukio na jinsi ya kufika sehemu husika pasipo kuzima simu yake ya mkononi. 

Pia alitoa wito kwa wananchi kuelewa manufaa ya uwekaji wa vifaa vya kuzimia moto katika majumba yao ili kupambana na majanga ya moto unapotokea.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA! 
(HABARI/PICHA : DENIS MTIMA/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.