Monday, February 9, 2015

Anonymous

Mauaji: Mwanamke Auawa kwa Kupigwa Risasi Tumboni Huko Kahama

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu.
Mwanamke aitwaye Mary Kashindye(45) mkazi wa kijiji na kata ya Mangolo tarafa ya Kahama mjini wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa risasi tumboni na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SS Longinus Tibishubwamu amesema mwanamke huyo aliuawa akiwa nyumbani kwake jana.

Amesema chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa ni ugomvi wa kiwanja baina yake na Jumanne Maige ambaye ndiyo anatiliwa mashaka na mwenzake Abdallah Kashindye.

Amesema jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano utakaofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa.

Tukio hilo linakuja siku moja tu baada ya miili ya watu watatu akiwemo mganga wa kienyeji kukutwa imeharibika vibaya ndani ya nyumba kutokanana kilichodaiwa kuwa waliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika katika kijiji cha Bugogo kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga. 
ZIMAMOTO YAZUNGUMZIA FAMILIA ILIYOTEKETEA KWA MOTO!===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA! 
-kadama malunde

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.