Monday, February 9, 2015

Anonymous

PICHAZ LIVE: WEMA SEPETU AKIFANYA YAKE NA MUME WA ZARI WA ZAMANI HUKO SOUTH AFRICA!

Kuanzia Kulia: King Lawrence, Ivan Ssemwinga na Wema Sepetu 
Ivan Ssemwanga, aliyekuwa mume wa Zari The Bosslady na aliyezaa naye watoto watatu ameanza kurusha mashambulizi kwa adui yake namba moja, Diamond Platnumz.

Mfanyabiashara huyo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini huenda akalipiza kisasi kwa Diamond anayetarajia kupata mtoto wake wa kwanza kutoka kwa Zari kwa mbinu ya ‘jino kwa jino’ ama zile za ‘kama noma basi iwe noma’.   

Picha liko hivi, Wema Sepetu kumbe yupo nchini Afrika Kusini ambako hata hivyo hatufahamu ameenda kufanya nini. Mshkaji wa karibu wa Ivan, King Lawrence (Yule mchizi aliyempa ofa Diamond ya $40,000 ili aachane na Zari), ameshare picha kwenye mtandao wa Instagram akila bata na Wema huku Ivan akiwpo pia.

Kuanzia Kushoto: Wema, Ivan na Lawrence akiwa na demu wake
Kwenye picha hizo, Lawrence anaonekana akiwa amekaa juu ya mapaja ya msichana asiyejulikana na pembeni yake yupo Ivan huku Wema aliyevaa kigauni kifupi cheusi akiwa kulia kwake.   

Lawrence pia amepost video kadhaa akiwa kwenye club hiyo na kuziandika ujumbe wa mfumbo ambao unaeleweka wazi kuwa unawaendea Zari na Diamond. “Rich Gangstas – What goes around comes around,” ameandika. “Oh Z*** get out of the way,” ameandika kwenye video nyingine ambayo unasikika wimbo wa Ludacris, Move Bitc*.

Awali Lawrence alipost picha nyingine hiyo chini akiwa kwenye eneo lile lile ambalo Wema alipiga picha.

Ni mapema sana kuhitimisha kuwa Ivan anataka kulipiza kisasi kwa Diamond kwa kumchukua Wema, lakini ni wazi kuwa kambi yake inataka kupeleka ujumbe ulio wazi kwa Chibu kuwa ‘vita imeanza’.
Acha project iendelee…
PICHAZ: POZI TATA ZA KIMAHABA ZA MTOTO MZURI BATULI NA KUDUME MMH...! 
===>>JIONEE HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.