Akizungumza leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini Dar e s Salaam, amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu kunaweza kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi, vifo na kadhalika.
Alisisitiza waache kuandamana ingawa dhamira yao ya kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa upigaji kura kutoka siku saba hadi 14 ina mantiki kwa Watanzania wote.
JIVICUF walikuwa waandamane kusisitiza, miongoni mwa mambo mengine, kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu nchini na dosari za uandikishaji wapiga kura.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU
TENA!
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)

Note: Only a member of this blog may post a comment.