Friday, February 6, 2015

Anonymous

NEW UPDATES: LICHA YA UTATA HATIMAYE GHANA YAWAFUATA IVORY COAST FAINALI AFCON 2015

Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Afcon baada ya kuwafunga wenyeji Equatorial Guine akatika mchezo wa nusu fainali uliopigwa usiku huu (Alhamis). 

Ghana wakiingia kwa kujiamini baada ya kuwatoa Guinea katika hatua ya robo fainali walianza kuonyesha dhamira yao mapema wakishambulia lango la wapinzani wao kwa nguvu na walipata bao mapema kwenye dakika 42 mfungaji akiwa Jordan Ayew ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya kipa wa Equatorial Guinea kumchezea vibaya Kwesi Appiah. 
Ghana walifunga bao la pili kupitia kwa Mubarak Wakaso  ambaye alifunga kwenye dakika ya 46 baada ya kupokea pasi toka kwa Christian Atsu . 

Nahodha wa timu hiyo katika mchezo huo Andre Ayew ambaye alikuwa anshikilia nafasi ya Asamoah Gyan alifunga bao la tatu kwenye dakika ya 75 na kuua matumaini ya Equatorial Guinea kucheza fainali . 

Mchezo huo ulilazimika kusimama kwa muda baada ya mashabiki wa Equatoarial Guinea kuanza kufanya vurugu wakionyesha hasira zao baada ya kufungwa . 

Ghana ambao wameingia kwenye fainali yao ya kwanza tangu mwaka 2010 watakutana na Ivory Coast katika mchezo wa fainali utakaopigwa jumapili ijayo huku Equatorial Guinea wakicheza mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo siku ya jumamosi.

Mechi hiyo ilizua zengwe dakika ya 82 baada ya vurugu kubwa kutokea na kusabisha mechi kusimama kwa takribani dakika 20. Ajabu baada ya sehemu kubwa ya mashabiki kutoka uwanjani na vurugu kutulia mechi iliendelea ila ikiwa dakika ya 90 na kuongezwa dakika 3 tu za nyongeza! 

Hali hii imezua sintofahamu kubwa kwa mashabiki kwa mara nyingine kufuatia lile zengwe la kufuzu kwa bahati nasibu lililoindoa Mali mashindanoni! 
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
 KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.