MSHTUKO! MAMA KANUMBA ANA LAANA!
Stori: Laurent Samatta/Risasi
BABA
wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amemchana mzazi mwenzake,
Flora Mtegoa kuwa anateswa na laana na ndiyo maana hafanikiwi.
Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba.
Mzee huyo alisema mama Kanumba ameshindwa kufanikiwa katika mambo
mengi likiwemo suala la kuendeleza ofisi ya marehemu kutokana na
kushindwa kumshirikisha yeye kama baba na ndiyo maana amepata laana.
“Tatizo ni papara ya mwezangu ya kutaka mali ndiyo mambo yanayotokea
na kamwe hataweza kufanikiwa kwa sababu baraka za mtoto zinatoka kwa
mama na baba na hiyo laana itazidi kummaliza sababu hakunishirikisha,”
alisema.
Mama Kanumba Flora Mtegoa.
Alipotafutwa mama Kanumba kuhusiana tuhuma hizo, alisema:
“Huyo
mzee yeye ndiyo ana laana, nimeshamzoea, hana jipya amekalia majungu.
Mimi sina laana, nakaa kwenye nyumba ya maana na si kama yeye anayeishi
kwenye nyumba ya udongo.”
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU
TENA!
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
WASANII
on Saturday, February 14, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.