Monday, February 9, 2015

Anonymous

LOVE YA UKWELI: SAMUEL KUFFOUR ANYOLEWA NYWELE LIVE BAADA YA GHANA KUFUNGWA NA IVORY COAST!

Mchezaji wa zamani wa timu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ghana Samuel Osei Kuffour ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha television cha Super Sport, amenyoa nywele zake baada ya timu ya Taifa ya Ghana kufungwa kwa changamoto za mikwaju ya penati kwenye fainali ya AFCON 2015.

Kuffour alitabiri kuwa Ghana wangeibuka na ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast na kama wasiposhinda basi anyolewe nywele zake.

“Mleteni kabisa kinyozi kwenye jumba hili kubwa, ili Ivory Coast wakishinda aninyoe nywele zangu zote,” Kuffour alisema kabla ya mechi kuanza.

Na baada ya mechi kumalizika na Ivory Coast kushinda kwa penati 9-8 dhidi ya Ghana ndipo mtangazaji mmoja akachukua mashine ya kunyolea na kuanza kunyoa Kuffour.
Mauaji: Mwanamke Auawa kwa Kupigwa Risasi Tumboni Huko Kahama!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA! 

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.