SIKU chache baada ya kuvuja kwa picha zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari
aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi
kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana. Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayehiheshimu kwa sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume gani amuoe lakini nahitaji
mtu mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe ndio anaweza kuwa baba wa
familia la sivyo inakuwa ni mambo ya kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa
Diamond.” Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli hiyo ya mama Wema, simu yake iliita bila kupokelewa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia picha ya Zari huku akizungushia duara tumboni na kuandika; ‘kileee kinaanza kumharibia mtu mavazi.’
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.