Saturday, February 14, 2015

Anonymous

KIVAZI CHA NUSU UTUPU CHA LULU CHAZUA BALAA BAR! APEWA ZA USO NA VIDUME!

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya/Risasi 
MTANGAZAJI na muigizaji wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amezua tafrani la aina yake baada ya kutinga kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar akiwa nusu utupu.
Mtangazaji na muigizaji wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo Lulu alipoingia alipita katikati na kwenda katika kaunta ya baa hiyo huku akijitingisha makusudi na kusababisha wanaume waliokuwa wamekaa kwenye baa hiyo wapige kelele wakimtaka aondoke. 

“Hii sasa ni sifa haiwezekani atuvalie kigauni kifupi namna hii, akibakwa atasemaje? Hatukubali, bora ingekuwa usiku, tumwambie mwenye baa kama anataka amtoe huyu au sisi tuondoke, hata kama tuko baa lakini tunajieheshimu,” alisikika mmoja wa wanaume hao. 

“Huu ujinga bwana sisi tunajiheshimu, hawezi kuvaa hivi tena inaonesha hana hata kufuri, bora niondoke eneo hili,” alisikika mwanaume mwingine na kuondoka zake.Hata hivyo, meneja wa baa hiyo aliwasihi watu kubaki na kumvumilia lakini wengi wao waliamua kuondoka kwa hasira. 

Waandishi wetu walipomuuliza sababu ya kufika pale na kiguo hicho alisema kuwa alifika kwa mambo yake muhimu na kukutana na rafiki zake Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha hivyo kama wateja wengine wamemsusuia, watajijua.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.