Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki na kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Suleimani Omari mbele ya hakimu Halfani Ulaya.
Mbele ya Hakimu Halfani Ulaya, Mwendesha Mashtaka Suleimani Omari alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto wake Februari 5 mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake huko katika mtaa wa Migongo.
Suleimani alidai kuwa mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti amekuwa akimlawiti mtoto huyo huku akimpa vitisho vya kwamba endapo angethubutu kutoa taarifa hizo kwa majirani, basi angeweza kuondoa maisha yake ili aweze kuepukana na aibu hiyo.
Alisema siku ya tukio mtuhumiwa huyo alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na ndipo alipomvamia mtoto huyo na kuanza kumlawiti na ndipo mtoto huyo alianza kupiga makelele ya kuomba msaada lakini kwa bahati mbaya hakuna jirani hata mmoja aliyeweza kusikia sauti za mtoto huyo na alifanikiwa kukimbia na kulala vichakani.
Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa asubuhi mtoto huyo alikuwa ameumizwa usoni pamoja na mgongoni kutokana na kipigo alichokuwa amekipata usiku na kwamba alipoulizwa na watoto wenzake kwa nini ana majeraha aliwaeleza amepigwa usiku na baba yake alipokuwa akijaribu kujiokoa wakati akimlawiti.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.