BONDIA bingwa wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka ambaye juzi alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kumpiga mtu ngumi, alihenyeshwa kiasi cha kutosha kabla ya kupandishwa kwenye karandinga la Magereza lililompeleka kuanza maisha mapya katika gereza la Manispaa ya mkoa.
Awali, baada ya hukumu hiyo, Cheka alipelekwa katika chumba ambacho mahabusu hukaa kusubiri kuondoka na akiwa huko, alionekana akikabidhi baadhi ya vitu alivyokuwa navyo kwa ndugu na jamaa zake.
Bondia bingwa wa dunia wa WBF uzani wa Kati, Francis Cheka akiwa chini ya ulinzi mkali.
Wakati akiondolewa kwenda kupanda gari,
Cheka alichukua simu yake na kuwapigia baadhi ya marafiki zake
kuwajulisha juu ya msala huo, lakini Polisi hawakumruhusu kuendelea na
jambo hilo, kwani walimnyang’anya na kumpeleka garini, ambako aliungana
na mahabusu pamoja na wafungwa wengine.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa Cheka waliokuwepo mahakamani hapo, waliangua kilio baada ya hukumu hiyo, akiwemo mkewe ambaye inasemekana kuwa ni mgonjwa. Mdogo wake naye aliangua kilio kikubwa kiasi cha kusaidiwa na meneja wa bondia huyo.
Cheka akichukuliwa na mahabusu wengine kwenye karandinga kwenda kuswekwa lupango.
Wakizungumzia hukumu hiyo, baadhi ya wakazi wa mjini hapa walisema
Cheka aliichukulia kirahisi kesi hiyo na ndiyo maana amehukumiwa, kwani
tokea kuanza kwake, hakuwahi kupeleka shahidi na hata siku ya hukumu,
alishindwa kutoa utetezi wowote.
MAJONZI! AJALI YA MOTO NYUMBANI KWA MSANII BELA!
===>>SHUHUDIA HAPA!
PATA HABARI HARAKA ZITUFIKIAPO.
===>>SHUHUDIA HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
ASANTE NA KARIBU TENA!

Note: Only a member of this blog may post a comment.