ALIYEKUWA meneja wa baa ya Vijana Social ya mjini
Morogoro iliyokuwa ikimilikiwa na Bondia Francis Cheka, Bahati Kabanda
aliyemponza hadi kuhukumiwa kifungo, hivi sasa anaishi kwa hofu kutoka
kwa mashabiki wa bingwa huyo wa masumbwi wa dunia.
Aliyekuwa meneja wa baa ya Vijana Social ya mjini Morogoro.
Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga ngumi na kumuumiza meneja wake
huyo, wakati alipokwenda kwa ajili ya kufuata fedha za mauzo ya baa yake
hiyo lakini wakapishana maneno yaliyosababisha tukio hilo lililowashtua
watu wengi.
Bondia
Francis Cheka (kulia) akiwa amepanda ndani ya gari la polisi baada ya
kuhukumiwa miaka mitatu jela kwa kumpiga meneja wa baa yake ambapo
atamlipa fidia ya sh. milioni moja. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya
Hakimu Mkazi ya Morogoro.
Licha ya mashabiki wa bondia huyo aliyemaliza enzi za Snake Boy,
Rashid Matumla, watu wengine wanaodaiwa kumpa hofu Baraka ni pamoja na
wakusanya chupa za plastiki ambao walimtegemea Cheka kwa ajili ya kwenda
kuziuza katika kiwanda chake kilichopo maeneo ya Kihonda mjini hapa.
...Akipanda gari kwenda jela.
“Ukweli maisha ya huyu jamaa hapa Morogoro ni magumu sana kwa sababu
kila anakokwenda anakutana na watu wanaomnanga juu ya kitendo
alichokifanya. Watu wanaomtakia mema wanamshauri kuwa mwangalifu sana wa
nyendo zake kwani watu wanaweza kumfanya lolote maana Cheka ni mtu
muhimu sana hapa,” alisema shuhuda mmoja.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!
-GPL
Note: Only a member of this blog may post a comment.