Friday, February 6, 2015

Anonymous

20 PICHAZ: AIBU! TASWIRA YA VURUGU ZA MASHABIKI WA EQUATORIAL GUINEA ZILIZOSIMAMISHA MECHI YAO NA GHANA AFCON 2015



MECHI ya pili ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea jana usiku ilivurugika baada ya mchezo huo kusitishwa kwa zaidi ya dakika 30 kutokana na ghasia za mashabiki.

Mashabiki waliokuwa jukwaani waliwarushia chupa za maji wachezaji waliokuwa uwanjani huku polisi wa kuzuia ghasia sambamba na helikopta iliyokuwa ikiruka juu ya uwanja wakijaribu kuwatuliza mashabiki hao. 

Vurugu uwanjani hapo zilikithiri katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Ghana na Equatorial Guinea. 

Mpaka vurugu zinatokea uwanjani hapo, Ghana tayari ilikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0 ambapo kwa matokeo hayo, Ghana imetinga fainali na itacheza dhidi ya Ivory Coast siku ya Jumapili. 

Ushindi huo wa Ghana haukuwafurahisha mashabiki wa wenyeji, ambao walikuwa na matumaini makubwa kuona timu yao ikicheza fainali dhidi ya Ivory Coast. 

Ghana ilianza kujipatia mabao yake kupitia kwa Jordan Ayew akifunga katika dakika ya 42 kwa njia ya penalti, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andre Ayew akitupia la tatu katika dakika ya 75 ya mchezo. 
 
Bao hilo la tatu ndilo lililozidisha fujo uwanjani hapo kwa mashabiki wa Equatorial Guinea kuwarushia chupa za maji wachezaji kiasi cha mpira huo kusimamishwa kwa muda mrefu














SAMAHANI KWA PICHA: MWANAJESHI AUAWA KIKATILI NA RAIA JIJINI MBEYA, KISA MKE WA MTU!
===>>SHUHUDIA HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA! 

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.