Mwanamuziki Hussein Machozi akiwa kimahaba na mchepuko wa Kizungu.
Na Musa Mateja
Baada ya mwanamuziki Hussein Machozi kudaiwa kumtelekeza mkewe aliyemuoa nchini Kenya, hivi karibuni picha yake imenaswa akiwa kimahaba na mchepuko wa Kizungu.
Baada ya mwanamuziki Hussein Machozi kudaiwa kumtelekeza mkewe aliyemuoa nchini Kenya, hivi karibuni picha yake imenaswa akiwa kimahaba na mchepuko wa Kizungu.
Picha hiyo inamuonesha Hussein akiwa kifua wazi huku mwanamke huyo
akimchezea kifua sambamba na kumng’atang’ata shingoni na Ijumaa
liliipata kupitia kwa rafiki wa msanii huyo aliyeomba asitajwe.
“Huyo Mzungu ndiye anatoka na Hussein kwa sasa ila zaidi mtafutani mwenyewe,” alisema mtoa habari huyo kwa ufupi.
Hussein Machozi akiwa katika pozi.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo Ijumaa lilimtafuta Hussein na alipopatikana alifunguka:“Huyu Mzungu ni mtu wangu kweli na tuna mipango yetu ila siyo muda muafaka kuianika, lakini nyie mmeipata wapi? Kama vipi ichunieni.”
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.