Thursday, December 22, 2016

Unknown

Mabingwa wa EPL, Leicester City Washinda Tuzo Hii Uingereza!

Klabu ya Leicester ambao ni mabigwa watetezi wa ligi kuu Uingereza imefanikiwa kushinda tuzo ya timu bora ya mwaka.
The Foxes kama wanavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo.
Kocha wa Leicester Claudio ranieri alishinda tuzo ya kocha bora wa mwaka Uingereza
Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa katika ligi ya Uingereza mwaka 2014-15.
Walipoteza mechi tatu pekee katika msimu wa 2015-16 na wakafanikiwa kushiriki michuano ya vilabu bingwa Ulaya na kuendelea hadi raundi za muondoano.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.