Mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku anatarajia kupewa mkataba mpya na klabu hiyo ya Everton ambao atakuwa akilipwa pauni 100,000.
Everton ambayo uwanja wake wa nyumbani ni Goodison Park ambao upo jijini Liverpool, haijawahi kutoa pauni 100,000 kwa mchezaji yoyote.
Lukaku ambaye alijiunga na Everton Juni, 2019 akitokea Chelsea na imeelezwa wakala wake Mino Raiola amekuwa katika mazungumzo mazito na uongozi wa Everton.
Majira ya joto, nusura Lukaku arejee tena Chelsea lakini suala hilo lilishindikana baada ya mwekezaji mpya wa Everton, Farhad Moshiri kusisitiza anataka bado aendelee kubaki.
Note: Only a member of this blog may post a comment.