Wednesday, December 21, 2016

Unknown

Baa za Zanzibar Kufunguliwa Kwa Saa Nne Tu!

Yawezekana wewe ni mmoja wa wanaotamani kwenda kupumzika kwenye visiwa vya marashi ya karafuu Zanzibar kwani wengi hupenda kufanya utalii visiwani humo kutokana na mengi mazuri yanayopatikana ndani ya visiwa hivyo.

Sasa taarifa ikufikie kwa wewe mpenda starehe hususan wale wanaopenda kutembelea maeneo ya baa kwamba kwa sasa baa za Zanzibar zitafanya kazi kwa saa nne pekee ndani ya siku, yaani kuanzia saa kumi jioni hadi saa mbili usiku na hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Uwanja wa Amani baada ya kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ongezeko la wimbi la madada poa.

Amri hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo imemgusa Mwenyekiti wa Kamati za Baa Zanzibar Hussein Ali Kimti na kusema kitendo cha kupunguza muda wa saa zao za kazi kutapelekea ugumu mkubwa wa maisha yao ya kila siku kwani ni wazi kipato chao kitaporomoka kwa kasi.

Lakini pia Mwanasheria wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Vyakula na vinywaji Zanzibar, Hassan Cornel amesema agizo lililotolewa na mkuu huyo wa mkoa ni zito kwa wafanyabiasahra hao kwani wamekuwa wakilipa kodi hivyo amemtaka kuweka mikakati mizuri ili kuendana na mazingira ya kodi zao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.