Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewafukuza chuo walimu wanafunzi watatu kwa tuhuma za kumpiga mwanafunzi Sebastian Singuli wa Shule ya Sekondari Mbeya Day. Profesa Ndalichako amesema kwa mujibu taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanywa na wanafunzi hao ni kosa la jinai na hawawezi kuendelea na taaluma ya ualimu kwa sababu wamekosa sifa ya kuwa walimu.
Mpaka sasa Mkuu wa Shule na baadhi ya walimu wamefikishwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Aidha Prof Ndalichako ameelezea kusikitishwa kwake pamoja kuchukizwa na kitendo hicho ambacho amesema si cha kawaida na hakiwezi kufumbiwa macho katika jamii.
Aidha Prof Ndalichako ameelezea kusikitishwa kwake pamoja kuchukizwa na kitendo hicho ambacho amesema si cha kawaida na hakiwezi kufumbiwa macho katika jamii.
– TBC
Note: Only a member of this blog may post a comment.