Msanii wa WCB, Raymond, amedai kuwa wakati mwingine anapofuata sana misingi ya kazi, baadhi ya watu hudhani kuwa anaringa, kitu ambacho anadai hawezi kuwa nacho.
“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi sababu ndio unaonipa hela,” aliongeza.
Muimbaji huyo ametajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha Best Breakthrough Act
-Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.