Habari zilizoifikia ambazo hazijathibishwa na TFF, Bodo ya ligi wala chama cha waamuzi ni kwamba, mwamuzi wa kati Martin Saanya na msaidizi wake namba moja (line one) Samwel Mpenzu, wamefungiwa miaka miwili kuchezesha soka.
“Martin Saanya na Samwel Mpenzu wamefungiwa miaka miwili lakini line two Ferdinand Chacha yeye amesalimika,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutoandikwa jina.
“Kadi nyekundu aliyooneshwa Jonas Mkude imefutwa baada ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa kadi hiyo ilitolewa kimakosa.”
Baada ya mchezo wa Yanga vs Simba, kuliibuka mijadala mingi na mikubwa juu ya mwamuzi Martin Saanya kulikubali goli la Tambwe ambaye aliushika mpira kabla hajafunga huku Samwel Mpenzu akilaumiwa kwa kulikataa goli la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa madai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.
Note: Only a member of this blog may post a comment.