Wiki hii tunaye mwanadada anayeunda Kundi la Navy Kenzo anayefahamika kwa jina la Aika Mariale. Huyu ni mpenzi wa mwanamuziki na prodyuza aitwaye Nahreel. Amefunguka mambo mengi kuhusu usanii na maisha yake ya kimapenzi. Ungana na Mwandishi Wetu Hamida Hassan aliyembana kwa maswali 10.
Ijumaa: Kwa nini uliamua kumkabidhi moyo wako Nahreel na si mwanaume mwingine?
Aika: Ni mapenzi yangu kwake tu, si unajua tena kipenda roho!
Ijumaa: Wewe na mpenzi wako mmedumu kwa muda mrefu, vipi suala la ndoa na mtoto?
Aika: Ishu ya ndoa bado hatujapanga ila hilo la mtoto naamini tutampata Mungu akipenda.
Ijumaa: Je, Nahreel akikutamkia ndoa utataka akulipie mahari ya shilingi ngapi?
Aika: Mimi mahari sitaki, kwetu hamna utaratibu huo.
Ijumaa: Ina maana utaolewa bure? Au ndiyo mambo ya huruma tena?
Aika: Hapana, huo ni utaratibu wa familia yetu. Mambo ya mahari huwa hatuna.
Ijumaa: Wewe ni msanii na unafanya kazi na mpenzi wako, je ni changamoto zipi unazipata?
Aika: Changamoto ni za kawaida, upo usumbufu wa wanaume ambao wala haunisumbui, najiheshimu na naheshimu kazi pia.
Ijumaa: Mmedumu kwenye penzi kwa miaka takriban 16, nini siri ya mafanikio?
Aika: Ni kuelewana na mpenzi wangu, wakati mwingine kujishusha hata kama yeye ndiyo kakosea, kujua nini usifanye kumuudhi mwenzako na kumpenda pia.
Ijumaa: Je, unapenda kumpikia chakula gani?
Aika: Anachokipenda hasa makaroni ya Cheese na nyama ya kusaga.
Ijumaa: Mastaa huwa wanasumbuliwa sana na wanawake, siku mpenzi wako akikusaliti utafanya nini?
Aika: Kitakachofuata ni kumuacha tu maana huenda ameamua kuhamishia mapenzi kwa mwingine.
Ijumaa: Kuna kukoseana kwa hapa na pale, kwa mfano mpenzi wako akikukosea, akufanyie nini ili uwe sawa?
Aika: Kikubwa aniombe msamaha tu na kuniahidi kutonikwaza tena.
Ijumaa: Ukipata mtoko na baby wako unajisikia poa mkienda wapi? Huwa unavaaje?
Aika: Napenda kwenda kuangalia muvi, kuogelea na mavazi yangu huwa ni simpo tu. Jeans na vitop kwa sana.
Ijumaa: Mbali na muziki unajihusisha na nini kinachokuingizia kipato?
Aika: Ukiacha muziki, mimi ni mjasiriamali pia.

Note: Only a member of this blog may post a comment.