Video ya wimbo ‘Salome’ ya Diamond Platnumz na Raymond imefikisha views milioni tatu katika mtandao wa YouTube kwa kipindi cha wiki moja.
Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameandika:
3 Million Views Now!!!!! Kwa mapenzi mnayo ionyesha Nyimbo hii Kwakweli sina cha kuwalipa zaidi ya kuwashukuru na kuwaombea kwa Mwenyez Mungu awafungulie kila jema mliombalo… Nawashkuru sana🙏 …..
Hii ni hatua nzuri kwa muziki wa Tanzania, kwani inaonyesha ni jinsi gani watanzania wameamka kusupport muziki wenye vionjo vya nyumbani.


Note: Only a member of this blog may post a comment.