Kama akikosa urais wa Marekani, Donald Trump anasababu chungu mzima za kujilaumu kutokana na kutumia fedha nyingi huku jarida la Forbes likiripoti kuwa mfanyabiashara huyo amepoteza zaidi ya $800 milioni kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo jengo lake la pili kwa urefu la San Francisco limedaiwa kupanda thamani kati ya majengo saba yaliyotangazwa kupanda thamani.
Mpaka sasa inakadiriwa mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican ameshatumia zaidi ya kiasi cha $55 milioni kutoka mfukoni kwake kwenye kampeni hizo.
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa kama vile NBC Universal, Univision na Macy’s.
Lakini Forbes wanadai kuwa utajiri wa Trump ni dola bilioni 3.7 huku vyanzo vingine kama Bloomberg kimedai kuwa ana utajiri wa $3bn nao Fortune wanasema ana $3.9bn.
Note: Only a member of this blog may post a comment.