Stori: Imelda Mtema, Wikienda
DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan amempongeza
‘kumpa tano’ Mtangazaji wa Kipindi cha Mboni Show kupitia TBC1, Mboni
Masimba kwa kuwakusanya watoto yatima wa vituo mbalimbali jijini Dar
kisha kuwafuturisha akimwambia kuwa amejumuika naye kwa roho safi
aliyoionesha.
“Nampongeza sana Mboni ni wachache sana
wanaoweza kujitoa kufanya jambo kwa ajili ya watoto yatima, Mboni ni
mfano wa kuigwa,” alisema Mama Samia.
Mbali na Mama Samia, futari hiyo
ilihudhuriwa na viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, mabalozi wa nchi mbalimbali na
baadhi ya mastaa wa Bongo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.