DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa
mtangazaji wa matukio mbalimbali ya runingani Bongo, Pennieli Mungilwa
‘Penny’ (jina limehifadhiwa) amemjia juu mwanaye huyo baada ya kukerwa
na kitendo chake cha kujitoboa pua na kuweka kipini hivyo kumpa masharti
ya kukiondoa mara moja.
Akizungumza na Wikienda, Penny alifunguka kuwa alipoweka kipini hicho alijua kitakuwa ni kizuri na ni moja ya urembo anaoupenda lakini kwa bahati mbaya, mama’ke hakufurahishwa nacho hivyo ameamua kukiondoa na kuacha tundu lizibe.

“Sikujua kama nitamuudhi mama hivyo aliponiambia nikiondoe, sikuona sababu ya kuking’ang’ania,” alisema Penny.
Note: Only a member of this blog may post a comment.