Jokate Mwegelo ‘Kidoti
Nicodemus Jonas, Dar es SalaamMUINGIZAJI na mwanamitindo nchini, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameamua kuwa mstari wa mbele katika kampeni ya kupambana na vita ya ugonjwa hatari wa Endometriosis.
Kidoti amekubali kuwa balozi katika harakati hizo zinazoendeshwa na Taasisi ya Millen Magese (MMF) chini ya mlimbwende, Millen Happiness Magese katika kupaza sauti ya kutoa elimu juu ya ungonjwa huo ambao umekuwa ukiwasumbua wanawake.
“Kila mmoja anatakiwa kuguswa na tatizo hili, serikali ifanye kila linalowezekana katika kujua chanzo chake. Sisi wasanii tuna jukumu la kuwa mabalozi kutoa elimu juu ya ugonjwa huu nchini ili kuokoa mamia ya Watanzania,” alisema Jokate ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Jokate aliongeza kuwa, dalili za ugonjwa huo ni maumivu makali wakati wa hedhi, ambapo inakadiriwa watu milioni 176 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa huo akiwemo Millen.
Note: Only a member of this blog may post a comment.