Thursday, April 7, 2016

Anonymous

BUNGE LAAMUA WAFANYA BIASHARA YA NGONO KULIPA MILIONI 4

Biashara ya ngono imezidi kushamiri Duniani siku baada ya siku, hata hapa nchini mtembezi imeshuhudia serikali ikitoa matamko mbalimbali dhidi ya Biashara hiyo.

Lakini Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria mpya, inayopinga biashara ya ngono, hatua hiyo inadaiwa kwamba huenda ikaathiri maisha ya watu zaidi ya elfu thelathini ambao wanategemea shughuli za ngono katika kujipatia kipato ambao wengi wao ni raia wa kigeni.

Chini ya sheria hiyo mpya, watu watakaokutwa wakilipia huduma hiyo wataadhibiwa kwa kulipa dola 1,700.
Mmoja wa mbunge anayeunga mkono sheria hiyo ameitetea na kusema kuwa inalengo la kuhamasisha watu kujiondoa katika biashara hiyo.


Hata hivyo kundi dogo la makahaba waliandamana nje ya bunge wakipinga sheria hiyo kwa madai kuwa wapewe uhuru wa kujilinda wenyewe na si kukatazwa kufanya biashara hiyo.
Ni vyema serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikaiga mfano huo wa nchi ya Ufaransa na kuweka mikakati maalum itakayo pelekea watu kujiajiri.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.