Saturday, March 12, 2016

Anonymous

SIMBA SC: Haya Sasa, Chongeni Tena!

kiiza.jpgWachezaji wa Simba wakishangilia.
Said Ally, Dar, Derick Lwasye, Mbeya MJINI kuna habari kubwa tatu katika soka la Bongo, kwanza ni Yanga kutua Kigali kwa ajili ya kukipiga na APR lakini habari kubwa zaidi mpaka leo hii ni Simba kuipa kisago kikali Ndanda FC cha mabao 3-0 kisha kurejea katika usukani wa Ligi Kuu Bara, ya tatu utaisoma chini.
Simba ambao hawakuwa wakipewa nafasi ya kufanya vizuri katika ligi ya msimu huu kutokana na kuanza kwa kusuasua, wamerejea katika usukani wa ligi hiyo kutokana na ushindi huo walioupata jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam.
HAMISI-KIIZA
Kutokana na ushindi huo Simba sasa wamefikisha pointi 51 katika michezo 22, wakifuatiwa na Yanga yenye pointi 50 katika michezo 21, awali Yanga ilikuwa ileleni baada ya kuitandika African Sports mabao 5-0, Jumanne ya wiki hii kwenye uwanja huohuo.

Ushindi huo uliwafanya mashabiki wa Simba kutoka kifua mbele na kutamba kuwa wale wanaowasema wao kukaa kileleni kwa muda waendelee kusema kwa kuwa wao wanaufuata ubingwa kimyakimya.Kitendo cha Yanga kushika usukani Jumanne ya wiki hii na kuishusha Simba, kilisababisha utani uwe mwingi mitandaoni na mitaani ambapo mashabiki wa Yanga walikuwa wakiwaambia wenzao kuwa ‘bando lao la saa 24 limemalizika, ndiyo maana wamewaondoa kileleni’, lakini sasa Simba watakuwa na nguvu ya kujinadi ubora wao kutokana na ushindi huo wa jana.

Katika kipute hicho cha jana, Simba ilianza kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 36 kutokana na mabeki wa Ndanda na kipa wao, Jeremia Kisubi kujichanganya wakati Ibrahim Ajib alipopiga krosi.
Habari ya tatu kubwa mjini nayo inaanzia hapa, hii ni kutokana na mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza kufunga mabao mawili katika dakika ya 57 akiunganisha krosi ya Ajib na dakika ya73 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Danny Lyanga.
Kwa mabao hayo mawili, Kiiza amefikisha mabao 18 na sasa anaongoza katika msimamo wa wachezaji waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo akimzidi Amissi Tambwe wa Yanga ambaye ana mabao 17.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.