Thursday, March 17, 2016

Anonymous

Rais MAGUFULI Kavutiwa na Kipindi Cha Clouds 360 Mpaka Akaamua Apige Simu Hii Studio…

Kwenye zile kubwa ambazo zimenifikia leo March 17 ni pamoja na hii ya Rais wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuvutiwa na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv mpaka akaamua kuwapigia simu moja kwa moja studio na kuwapongeza.
Kingine alichokisema Rais Magufuli ni  kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kipindi hicho na anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Clouds Media Group kama zoezi zima la MalkiaWaNguvu na mengine mengi.
Rais Magufuli ambaye wakati anapiga simu studio alikua na Mke wake Mama Janeth Magufuli,amewapongeza Watangazaji wa kipindi hicho Hudson Kamoga,Babie Kabae na Sam Sasali,ambapo amepongeza namna ya uchambuaji wa Magazeti wa kipindi hicho.
Nimeinasa pia sauti ya Rais Magufuli akiongea live kwenye kipindi cha Clouds 360.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.