Kipaji cha Raymond
kilianza kuonekana mwaka 2011 baada ya kushiriki kwenye mashindano ya
kuchana yaani (FreeStyle) mkoani Mbeya na kuwa mshindi wa
kwanza,alipokuja Dar kwenye fainali za mashindano hayo akaibuka pia kuwa
mshindi ndipo Tip Top Connection ilipomchukua na kuwa chini yake.
Raymond ameshaoneka na kwenye majukwaa mengi hasa kwenye show za Madee,Kutokana na ukaribu wa Label ya TipTop Connection na WCB,Menejimenti zimekaa chini na kukubaliana kumtoa kupitia label ya Wasafi (WCB) ambayo uongozi wa label hiyo upo chini ya Diamond Platnumz.
Najua nina watu wangu ambao mlikuwa na hamu ya kufahamu vitu vingi kutoka kwa msanii huyo mpya kutoka WCB, sasa basi tazama hii video hapa chini Raymond akielezea alivyokutana na Diamond mpaka kusainiwa katika label ya WCB (Wasafi).
-via millardayo
Note: Only a member of this blog may post a comment.