Thursday, March 17, 2016

Anonymous

Pluijm: Tunawapa SIMBA SC Mechi Mbili Tu!


Wilbert Molandi, Dar es Salaam
WAKATI wapinzani Simba wakiongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm, ametamka kuwa hana hofu ya ubingwa huo.
Simba hivi sasa inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 54, Yanga 50, Azam FC 47 na Mtibwa Sugar 39.

Pamoja na Simba kuongoza lakini wamecheza michezo mingi kuliko wapinzani wao, wakiwa wamecheza michezo 23, Yanga 21 na Azam 20.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema kikubwa kinachompa jeuri ni idadi za mechi mbili alizozibakisha ambazo amepanga zote kushinda na kuhakikisha anawatoa kileleni Simba.
Pluijm alisema, katika mechi hizo zote atacheza kama vile fainali kuhakikisha wanalitetea taji hilo la ubingwa wanalolishikilia.

“Bado nina matumaini makubwa ya kurejea kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu, licha ya Simba kuongoza katika kipindi hiki ambacho tupo kwenye majukumu mengine ya michuano ya kimataifa.
“Hao Simba wenyewe wanaongoza ligi kuu kutokana na sisi kucheza mechi chache zaidi yao.
“Hivyo utaona ni jinsi gani bado tuna uhakika wa kurejea kileleni, kikubwa tutakachokifanya ni kila mechi kucheza kama fainali ili turejee kileleni,”alisema Pluijm.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.