UVUMI umeenea tangu mwishoni wa wiki iliyopita kwamba mwanamuziki
maarufu wa Nigeria, Peter Okoye, wa kundi la Psquare aliyeonekana
anatumbuiza peke yake, ni ishara ya mwanzo ya kuvunjika kwa kundi hilo
linaloongozwa na mapacha wawili.
Peter, ndugu yake, Paul, alifanya onyesho hilo kwenye klabu moja
jijini Abuja, Nigeria, alipopiga wimbo unaoitwa ‘Look into my eyes’
(Tazama machoni mwangu) ambapo watu wengi wanakisia huo ndiyo mwisho wa
kundi hilo la waimbaji hao.
Pamoja na yote hayo, pacha wake, Paul, aliandika katika ukurasa wake
wa Instagram kwamba anatamani mama yao angekuwa hai na kusaidia katika
mfarakano huo.
“Natamani ungekuwa hai, na sasa natambua maisha yalivyo bila ya kuwepo mama,” aliandika Paul.
Wakati huohuo, Jude, kaka yao na meneja wao wa zamani, pia aliandika kwenye mtandao huo kuwaomba mashabiki waendelee kutabasamu na bila kujali kitu.
Wakati huohuo, Jude, kaka yao na meneja wao wa zamani, pia aliandika kwenye mtandao huo kuwaomba mashabiki waendelee kutabasamu na bila kujali kitu.
Mashabiki waliozagaa duniani kote wanawaombea Psquare wamalize tofauti zao na waendelee na muziki wao.
Note: Only a member of this blog may post a comment.