Thursday, March 10, 2016

Anonymous

JE, WAJUA?! Kiswahili Fasaha Cha Maneno Yafuatayo: Kitchen Party, Smartphone, Expire, Live na Send-off party


Inawezekana Kiswahili ikawa ni lugha yako ya kwanza lakini bado kuna vitu vingi tu huvijui au huwa hauvitamki kwa Kiswahili ndio maana leo nimeamua kukutanisha na maana ya maneno machache ambayo tumezoea kuyatamka kwa kiingereza japo tunayaongea kwenye sentensi zenye kiswahili. 

Neno LIVE mfano pale unaposema CloudsTV inaonyesha LIVE… kwa Kiswahili LIVE ni PAPO, sasa hivi pia tunazo simu za kisasa ambazo tunaziita Smartphones ila kwa Kiswahili jina lake ni SIKANU……. pia kwenye ile sherehe maarufu kwa jina la Send-off kwa kiswahili ni ‘sherehe ya Mwago‘ kwa sababu Binti ndio anaagwa. 

Kuna kitu kinaitwa Kitchen Party ambapo kiswahili chake ni ‘JIKO MTAWAZO‘ yaani mtu anatawazwa kuhusu mambo ya jiko na mambo ya maisha ndio maana mtu akioa Waswahili wanasema umepata Jiko. 

Neno jingine la kufahamu kwa leo ni pale unapokuta kitu au bidhaa imekwisha muda wake wa matumizi mfano maziwa au mkate, neno maarufu tunalitumia ni ‘expire‘ ila kwa Kiswahili fasaha unaambiwa ni ‘IMECHOTORA

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.