Waandishi Wetu, Dar es Salaam
RAPA wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego katika moja ya
mashairi ya wimbo wake anasikika akighani: “Najisikia kuwachana” kisha
kuna watu wanaitikia: “Wachaneee!”
Sasa mashabiki na wadau wote wa soka wanatarajiwa kushuhudia kipute
cha timu kubwa katika soka nchini, Simba na Yanga, kesho Jumamosi ambapo
kipa upande umekuwa ukijinadi kuwa utawachanachana wapinzani.
Ni jambo la kawaida kwa mechi ya wapinzani hao kuwa na presha lakini
safari hii presha inaonekana kuwa kubwa zaidi kwa kuwa ubora wa
wachezaji hautofautiani kwa kiwango cha juu na kila upande umeonyesha
lazima upate ushindi, kinyume na hapo basi ujue litaibuka la kuibuka.
Wachezaji wa Ibrahimu Ajibu na Juuko Murshid (kulia) wakishangilia.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar, ambapo Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 45 katika michezo 19,
Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 katika mechi 18.
Kocha Simba amtaja anayemhofia
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda, amemtaja winga wa
Yanga, Simon Msuva ndiye anayemhofia kuelekea katika mchezo huo.
Kauli hiyo inaweza kuwashangaza wengi kwa kuwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma ndiyo washambuliaji wa Yanga ambao wameonekana kuwa na makali zaidi, lakini Mayanja yeye amemtazama Msuva katika jicho la tofauti.

Wachezaji wa Simba,(kutoka
kushoto), Hassan Isihaka,(wa pili kushoto) Haji Ugando, Mwinyi Kazimoto,
Ibrahimu Ajibu wakimpongeza, Hamis Kiiza(kushoto) baada ya kufunga moja
ya mabao dhidi ya timu ya Mgambo Shooting mchezo uliochezwa Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam jana. Simba ilishinda mabao 5-1.(Picha na Yusuf
Badi).
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mayanja kutoka
katika kambi ya Simba mkoani Morogoro, alisema: “Msuva ndiye mwenye
madhara na anayehitaji umakini katika kumchunga. Nimewaona Yanga katika
mechi kadhaa wametumia mawinga kupeleka mashambulizi.
“Nitahakikisha mawinga wao hawapati nafasi ya kupiga krosi kwa washambuliaji. Najua (Deus) Kaseke naye ni hatari lakini Msuva ndiye hatari zaidi.”
“Nitahakikisha mawinga wao hawapati nafasi ya kupiga krosi kwa washambuliaji. Najua (Deus) Kaseke naye ni hatari lakini Msuva ndiye hatari zaidi.”
Madee kumbe Yanga damu
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Hamad Ali ‘Madee’, amejinadi kuwa kikosi
cha Yanga ambacho yeye anakishabikia kipo fiti idara zote na haoni kama
Simba wanaweza kukwepa kupata kipigo.
“Ninajiamini tena sana, Simba atapigwa tu. Sawa, siku za karibuni wameonekana kuwa vizuri lakini bado Yanga ina kikosi bora.
“Ninajiamini tena sana, Simba atapigwa tu. Sawa, siku za karibuni wameonekana kuwa vizuri lakini bado Yanga ina kikosi bora.
“Mbele ukutane na Tambwe, Ngoma na Msuva ambao muda wote wana njaa ya
mabao, kati tunao kina Niyo na Kamusoko, Simba watatokaje?” alihoji
Madee na kuongeza:
“Pamoja na hivyo, bado namhofia Kiiza. Jamaa anajua na ninamkubali tangu akiwa Yanga na mpaka sasa bado namfuatilia kwa ukaribu.”
“Pamoja na hivyo, bado namhofia Kiiza. Jamaa anajua na ninamkubali tangu akiwa Yanga na mpaka sasa bado namfuatilia kwa ukaribu.”
Kavumbagu: Yanga watakaa
Straika wa Azam, Mrundi, Didier Kavumbagu, aliyewahi kukipiga Yanga, naye amefunguka kuelekea mchezo huo kwa kusema:
“Nafahamu mechi za Yanga na Simba hazitabiriki lakini hii ya Jumamosi naona Simba ina asilimia kubwa ya kushinda. Simba wanajiamini kwa kuwa wameshinda mechi sita mfululizo lakini pia kocha wao ni mtu anayelijulia sana soka la Afrika Mashariki.”
“Mayanja ataisumbua sana Yanga, namfuatilia tangu akiwa Rwanda, Uganda, Kenya na hata Kagera Sugar alikuwa na timu ndogo lakini alikuwa msumbufu sana.”

Kwa kuwa katika mchezo uliopita baina ya vigogo hao Yanga ilishinda
mabao 2-0 wafungaji wakiwa ni Amissi Tambwe na Malimi Busungu katika
dakika ya 44 na 79, wawili hao wamejinadi kurudia walichokifanya
Septemba 26, 2015.
“Tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi siku hiyo lakini natamani sana nirudie rekodi kama iliyopita ya kuifunga Simba katika dakika ya 79,” alisema Busungu.
Upande wa Tambwe alisema: “Mechi itakuwa ngumu lakini kabla kipindi cha kwanza hakijamalizika, tunatakiwa kuwamaliza kama ilivyokuwa mwanzo, namuomba Mungu anijalie hilo.”

Kurejea Dar
Katika kambi ya Simba iliyopo Morogoro, habari ni kuwa wachezaji wote
wapo fiti na madai kuwa Abdi Banda aliumia mazoezini imeelezwa kuwa siyo
kweli kwa kuwa mpaka jana jioni alionekana akiwa fiti pamoja na
wenzake.
Yanga ambao wapo Pemba kwa ajili ya kambi ya mchezo huo, wao wanaweza
kumkosa nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye hajawa fiti lakini
timu zote zimekuwa zikificha juu ya kurejea Dar. Imeelezwa kuwa Simba
walitarajiwa kurejea jana usiku huku Yanga wakitua leo Ijumaa kwa ndege
ya kukodi mida ya mchana.
Waandishi: Wilbert Molandi, Nicodemus Jonas, Hans Mloli na Sweetbert Lukonge

Note: Only a member of this blog may post a comment.