Wapendanao, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Kiba ‘King Kiba’ wakiwa katika pozi.
Na mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Wapendanao,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Kiba ‘King Kiba’, wamedaiwa kuzichapa
kavukavu ndani ya gari kisa kikiwa ni ujumbe mfupi wa maneno (SMS),
Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo
ilitokea katikati ya wiki iliyopita maeneo ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam bila kujulikana walikuwa wakitokea wapi kwenda wapi.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Jokate na Kiba awali walimwagana lakini
hivi karibuni wakarudiana baada ya familia ya Kiba, akiwemo mama yake,
kuwakutanisha Februari 5, mwaka huu kwenye Hoteli ya Slipway, Masaki
jijini Dar na kumaliza tofauti zao.
Siku hiyo ya kupatanishwa kulikuwa na
hafla ya uzinduzi wa video ya Kiba iitwayo Lupela ambayo inafanya vizuri
katika soko la muziki wa Bongo Fleva nchini.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Jokate na
Kiba walipishana kauli baada ya mrembo huyo anayefanya vyema katika
tasnia ya muziki, filamu na mitindo Bongo kulazimisha kusoma ujumbe
mfupi wa maneno ulioingia kwenye simu ya mpenzi wake huyo.
Ali Kiba ‘King Kiba’.
SIKU YA TUKIO
Chanzo hicho kiliweka bayana kuwa wawili
hao wakiwa katika mizunguko yao hivi karibuni, walisimamisha gari lao
maeneo ya Kinondoni-Biafra na ndipo walipoanza kuzozana kwa muda kabla
ya kuanza kushikana maungoni.
“Walitaitiana kwenye gari. Wakapaki,
Kiba alionekana kushuka kama anataka kumuacha Jokate peke yake ndani ya
gari, Jokate hakukubali, akashuka na yeye kumlazimisha arudi. Mazungumzo
yalisikika Jokate akihoji ni kwa nini jamaa anamkatalia kusoma meseji
iliyoingia kwenye simu yake! Ndipo timbwili liliponoga.
“Ilikuwa mtiti wa aina yake lakini Kiba
alipoona ‘nzi’ (mashuhuda) wanaanza kujaa, akaona isiwe tabu, akarudi
ndani ya gari na Jokate naye akaingia wakaondoka zao,” kilisema chanzo
hicho kilichoshuhudia timbwili zima.
MENEJA AFUNGUKA
Kabla ya kuwatafuta wawili hao,
mwanahabari wetu alimtafuta mmoja kati ya mameneja wa Kiba aliyeomba
hifadhi ya jina ambaye aliweka wazi kuwa, wawili hao walipishana
‘Kiswahili’ kutokana na SMS ambayo haikuwa mbaya isipokuwa walishindwa
kudhibiti hasira zao.
Msikie: “Walipishana lugha baada ya
Jokate kulazimisha kusoma au kuona ujumbe ulioingia kwenye simu ya
Kiba. Halafu kwani unafikiri basi ulikuwa ujumbe mbaya, ilikuwa ni
meseji yangu niliyomtumia kumpa maelekezo ya kazi lakini Jokate
akamaindi.
“Alichokosea Kiba ni kukataa kumpa simu
sasa sijui naye ana vimeo vyake au vipi lakini hapo ndipo utata
ulipoanzia. Wakavutana kwa muda lakini bahati nzuri Kiba akawa
mstaarabu, akarudi ndani ya gari kama Jokate alivyomtaka, wakamalizana
na kuendelea na safari yao,” alisema meneja huyo.
PENZI LIPO PALEPALE
Akaongeza: “Kwa sasa wapo freshi. Si
unajua mambo kama hayo kwenye mapenzi yanatokea. Wamewekana sawa na kila
kitu kipo kwenye mstari. Wamewekeana mikakati mizuri kuhusu matumizi ya
simu.”
KIBA ANASEMAJE?
Baada ya kuzungumza na meneja huyo,
mwanahabari wetu alimtafuta King Kiba kupitia kilongalonga chake cha
mkononi ambapo alipopatikana alitoa majibu tata ambayo gazeti
lilishindwa kubaini kama amekubali au amekataa.
Msikilize: “Kwa nini kila siku
mnaniuliza habari za skendo tu? Mbona hamniulizi kuhusu muziki wangu
unavyofanya vizuri kitaa au hujasikia ngoma yangu ya Lupela inavyokamata
chati? Acha mambo yako bwana.”
Akaongeza: “Halafu, hata kama ni kweli
wewe tatizo lako ni nini? Mengine ni mambo binafsi. Haipendezi kila
ninachofanya au kinachonitokea nikitangaze kwenye vyombo vya habari.
Mimi nafikiri uwe unaniuliza zaidi kuhusu kazi yangu ambayo mashabiki
ndiyo wanataka kuijua.” (akakata simu).
JOKATE HAPOKEI SIMU
Jitahada za kumpata Jokate ili aweze
kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya mrembo huyo kutopokea
simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu chochote.
Jokate na Kiba kwa sasa ni ‘kapo hot’
ambayo mashabiki wengi wanawaombea wafikie hatua ya kuoana licha ya kuwa
na mvutano kutoka kwa wazazi wa Jokate ambao waliwahi kuripotiwa
kutoafiki uhusiano huo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.