Magazeti ya Jumanne 11 August 2015
yako mtaani tayari yakiwa na vichwa vyake vya vikubwa vya habari, kazi
yangu ni kukusogezea uchambuzi wote wa magazeti na habari zake
zinazoweka headlines, baadhi zikiwa hizi kubwa…
John Magufuli asema ushindi wa CCM upo palepale waliohama wamekiacha Chama hicho kikiwa salama na mwaka huu watafanya kampeni za kisayansi, Mwigulu Nchemba asema ni rahisi sana kumnadi John Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Edward Lowassa alisimamisha jiji kwa masaa kumi ni safari kuelekea ofisi za NEC kuchukua fomu za kugombea Urais, shughuli za mahakama za simama, waendesha pikipiki wamsindikiza kwa mbwembwe na manjonjo.
Kundi la vibaka latikisa UKAWA, wafanya vurugu kwenye msafara wa Edward Lowassa, wavamia maduka, wapora mali za wafanyabiashara na wapita njia…Tafrani ofisi za NEC baada ya waandishi wa habari kuzuiwa kuingia ndani ya chumba cha kuchukua fomu ya Urais.
Dr. Mohammed Bilal akanusha uvumi wa kukihama Chama cha CCM...TCRA imetangaza kiama kwa watumiaji vibaya na wahalifu wote wa mitandao, watangaza Sheria ya Uhalifu ya Mitandao kuanza kutumika rasmi Septemba tarehe 1 mwaka huu.
Stori nyingine kwenye magazeti inasema, kanisa lawazuia zaidi ya waumini 4,000 haki za msingi za kujiandikisha na BVR, kuwa wanasiasa, kusoma zaidi ya darasa la saba na haki ya msingi ya kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Nimkuewekea sauti ya uchambuzi wote wa magazeti wa @Cloudsfm hapa chini.


Note: Only a member of this blog may post a comment.