UCHURO? Jokate
Urban Mwegelo ‘Kidoti’ ametabiri kile kinachoweza kuitwa ‘wosia wa kifo
chake’ kwa kuweka wazi mazingira ambayo angependa yafanyike siku
atakapotangulia mbele ya haki.
“Ishu ya atazikwa wapi anaiachia familia
yake. Lakini anapenda siku ya kuagwa aagwe kistaa (Leaders), watu wengi
wajitokeze,” alisema rafiki huyo.
Jokate ambaye ni Miss Tanzania Na. 2,
2006 pia mkurugenzi wa nembo ya Kidoti inayojishughulisha na urembo na
mitindo, anadaiwa amekuwa akijiuliza namna itakavyokuwa siku atakapoaga
dunia. Wakati mwingine anatamani angekuwa na uwezo wa kushuhudia.
Amani
lilimtafuta Jokate kwa njia ya simu na alivyopatikana alisema
ilivyoelezwa ndivyo angependa iwe na kwamba hakuna binadamu anayetamani
msiba wake uwe wa ajabu.
“Yeah! Mimi ni mtu wa watu, hadhi yangu
kwenye jamii unaijua, japokuwa ukweli unabakia kwamba muhimu ni matendo
mazuri, lakini hata hadhi ya mazingira ya msiba iwe nzuri kulingana na
utu.
“Napenda jeneza zuri, nyumba
nitakayopumzishwa (kaburi) iwe nzuri ili ibaki kumbukumbu kwa kizazi
kijacho kuwa Jokate aliishi akafanya hiki na hiki. Napenda watu wote
wahudhurie, mimi ni mtu wa watu. Ila wapi nizikwewazazi wangu wataamua,”
alisema Jokate kwa sauti ya utulivu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.